Kazi ya msingi katika nyumba

Msingi ni sehemu muhimu ya jengo ambayo huunganisha jengo na ardhi husika pamoja na kupeleka mzigo wa jengo kwa usalama kabisa katika ardhi. Pasipo msingi, jengo linakuwa halijakamilika na halipo salama. Kikawaida msingi hutumia gharama kubwa katika kujenga ukilinganisha na baadhi ya maeneo katika jengo, gharama hii kubwa inaashiria umuhimu na ulazima wa sehemu hii ya jengo.

Siku zote katika tathimini ya jengo, pale inapoonekana kuwa msingi ni mbovu, basi hatua za umakini zaidi huchukuliwa maana ipo hatari inayoweza kutokea na ikaleta hasara kubwa mpaka katika maisha ya watu; ni muhimu kuwa makini katika ujenzi wa msingi wa nyumba zetu ili kuweza kupunguza hatari ambazo zinaweza kutokea na pia kuongeza thamani na afya ya jengo lako.

Ufuatao ni mchanganuo unaoonesha faida na kazi ya msingi katika nyumba ili kuweza kukuongezea ufahamu zaidi katika ujenzi wako unaofanya.

Kupunguza ukubwa wa kanieneo wa jengo

Msingi huchukua uzito wa jengo zima na kuupeleka moja kwa moja katika ardhi kwa kuugawanya uzito huo katika eneo kubwa la ardhi ili kuweza kupunguza kiasi cha kanieneo (pressure) ambacho ardhi hubeba. Hii ni sawa na kuruhusu uzito mkubwa katika eneo moja kuweza kugawanywa katika eneo kubwa zaidi ili mwisho wa siku ardhi iweze kuhimili uzito wa jengo. Hii husaidia ardhi iweze kubeba kanieneo ambayo inaweza.

Ipo athari ambayo inaweza kutokea kama ardhi ikashindwa kubeba mzigo unaoweza; ardhi ambayo inabeba uzito kuliko uwezo wake huweza kupasuka na kaharibu jengo zima. Ni sawa na kamba ambayo imebeba uzito mkubwa kuliko uwezo wake, mwisho wa siku huishia kukatika na kuangusha mzigo wa thamani. Ni muhimu kuhakikisha kuwa mzigo ambao ardhi inabeba upo ndani ya kiwango kubalika. Kwa maeneo ambayo ardhi ni mbovu, basi utaalamu zaidi huhitajika ili kuweza kutengeneza msingi wenye uwezo wa kubeba uzito wa jengo salama. Uzito wa jengo ni jumla ya uzito wa jengo lenyewe, watumiaji na uzito wa nguvu ya upepo na nguvu nyingine zinazoweza kuliathiri jengo lako.

Jengo kukaa kwa usawa katika ardhi bila kushukia upande mmoja

Katika kipindi cha muda mrefu jengo lolote hushuka ijapo kidogo katika ardhi kutokana na hali ya ‘usponji’ ya udongo; inahitajika miaka kadhaa ili jengo lisiweze kushuka chini zaidi.  Kazi mojawapo ya msingi ni kuwezesha jengo kuweza kushuka katika ardhi kwa usawa bila kulalia upande mmoja; hii huwezekana pia kwa kuugawanya uzito wa jengo kwa usawa katika ardhi hivyo kama kushuka jengo, basi lishuke kwa pamoja pande zote.

Kama jengo likishuka upande mmoja sana na kulalia upande mmoja inaweza sababisha nyufa katika jengo zima na mwisho wa siku kulifanya liweze kuwa katika hali ya ubovu.

Ijapokuwa sababu ya jengo kushuka na kulalia upande mmoja huweza sababishwa na sababu nyingine, Lakini kama msingi wa jengo lako utaweza jengwa vyema basi utasaidia kuepusha madhara mbalimbali ikiwemo kulalia upande mmoja.

Msingi huweka sehemu iliyosawa na salama ya kujengea jengo

Msingi ni muhimu sana kwa kuweka sehemu ya kujengea iwe katika usawa mmoja ili kuweza kujenga jengo lako kwa usawa (level) kabisa. Mara nyingi ardhi ambayo tumekuwa tukiichagua kujengea inakuwa haipo katika hali ya usawa, inawezekana ipo katika mteremko au katika mawe; msingi husaidia kuweza kuliweka jengo lako katika sehemu iliyo salama bila kujalisha ardhi ipoje.

Tukifanikiwa kujenga msingi katika kingo za mito, katika bahari na katika maeneo yote ambayo ni hatarishi basi inakuwa ni hatua kubwa ya kutuwezesha kuliweka jengo letu katika eneo hilo. Msingi ndio hutengeneza sakafu iliyo sawa ya kujengea jengo lako na hivyo kuweza kuruhusu kufanya shughuli mbalimbali ndani ya jengo lako bila shida wala tabu.

Msingi hulitengemaza jengo lisiteleze, lisibinuke wala kuzungukia upande mwingine

Waweza kufikiri kuhusu habari ya jengo kuteleza, kubinuka au kuzunguka – ndiyo yawezekana ikatoke katika jengo kama halijajengwa vyema. Kama jengo likipigwa na upepo upande mmoja yawezekana likasukumwa upande mwingine; au kutokana na hali ya ardhi na mambo mingine inaweza kulifanya likatelezea upande mwingine kama halijajengwa vyema.

Msingi husaidia jengo lako likae sehemu moja iliyo salama. Msingi ni kama nanga ambayo huiifunga sehemu ya juu ya jengo iweze kuwa imetengemaa vyema. Pale upepo, tetemeko la ardhi linapoipiga nyumba yako basi bado itaendelea kuwa salama.

Msingi huilinda nyumba kutoka katika athari za kuchimbwa na kulika chini

Wapo wanyama na wadudu mbalimbali ambao huchimba ardhi na kusababisha mashimo chini ya nyumba. Wadudu kama mchwa, sisimizi; wanyama kama nyoka, panya, sungura, vicheche n.k huweza sababisha mashimo chini ya nyumba; na yanaweza leta athari kama nyumba haijajengwa vyema.

Nyumba kama imejengwa katika njia ya maji, basi maji hayo yanaweza kusababisha nyumba ilike na mwisho kuweza kuanguka na kuleta athari mbalimbali.

Msingi hujengwa kwa kuhakikisha kuwa jengo lote linakuwa salama na matukio ya kulika kwa ardhi na kuchimbwa kwa mashimo katika ardhi; hii inakwenda sambamba na kuhakikisha kuwa msingi unaendelea kulindwa na kufanyiwa matengenezo katika kipindi chote cha jengo.

Mwisho, ijapokuwa kujenga msingi ni gharama, bado ni muhimu kuhakikisha kuwa jengo lako unalijenga kwa umakini na nidhamu huku ukihakikisha msingi wako umejengwa kwa kufuata taratibu za kitaalamu. Ni muhimu kuhakikisha msingi wako hauna makosa na unafanya kazi vizuri; ni pamoja na kukumbuka kufanya matengenezo mbalimbali pale inapotokea shida fulani katika msingi wako. Linda msingi wa jengo lako ili jengo liendelee kuwa imara.

mangula
Eng. Makazi Team
Makazi.ne.tz ni mtandao mahususi Afrika Mashariki wenye lengo ...
ID-19368
4
193 sqm
133 Pcs
16 m
3,455 Pcs
15 m
1,718 Pcs
ID-16988
3
144 sqm
99 Pcs
13 m
2,578 Pcs
12 m
1,282 Pcs
ID-25326
6
442 sqm
0 Pcs
24 m
12,170 Pcs
22 m
4,332 Pcs
ID-17807
4
353 sqm
146 Pcs
16 m
9,354 Pcs
15 m
3,025 Pcs
ID-13047
4
135 sqm
94 Pcs
17 m
2,112 Pcs
9 m
921 Pcs
ID-16993
4
169 sqm
116 Pcs
15 m
3,025 Pcs
12 m
1,504 Pcs
ID-22334
3
178 sqm
122 Pcs
17 m
3,181 Pcs
15 m
1,582 Pcs
ID-27952
5
149 sqm
105 Pcs
15 m
2,700 Pcs
13 m
1,330 Pcs
ID-17589
3
129 sqm
89 Pcs
12 m
2,309 Pcs
12 m
1,148 Pcs
ID-18210
4
493 sqm
0 Pcs
21 m
15,400 Pcs
20 m
3,763 Pcs
ID-18083
3
158 sqm
70 Pcs
18 m
3,992 Pcs
12 m
1,406 Pcs
ID-18060
3
144 sqm
99 Pcs
13 m
2,578 Pcs
13 m
1,282 Pcs
Makazi Icon Blue

Jiunge Uanachama

Jiunge uanachama ili uweze ona ramani ya mpangilio vyumba kabla hujanunua ramani kamili; Fahamu inahitaji PESA kiasi gani KUWEKEZA ktk biashara yako ili faida yake uitumie kama mtaji wa kujengea nyumba hiyo. Fahamu kiasi cha MKOPO UJENZI cha kuchukua na kurudisha kila mwezi ktk benki yako. Pia, utaweza ona GHARAMA za kujenga msingi, kuta, paa, dari, rangi, milango, madirisha... kwa nyumba zote ktk mtandao wetu, ili uweze CHAGUA, LINGANISHA, KUWEKA MIPANGO & MIKAKATI ya Jinsi ya Kuuendea Ujenzi Wako Vyema!