Punguza 5% ya gharama ya ufundi kisha utapewa QUOTATION YA VIFAA vinavyohitajika kwa steji hiyo uliyochagua; Utatumiwa ndani ya lisaa limoja ktk email na pia tutakupigia simu
Ukishapewa quotation ya vifaa, basi utatujuza siku gani fundi wetu aje kwako kukujengea kwa steji hiyo (Atakuja siku 3 tangu umuite kama upo mkoani)
Ili Fundi aje unapaswa uweze kumalizia 95% ya ada ya ufundi iliyobaki hapa hapa mtandaoni
Kwa Boss uliye mkoani utawajibika kwa swala la nauli ya fundi kuja na kurudi. Nauli zimeorodheshwa hapo juu
Kazi inapoendelea site, tunaendelea kuwasiliana na fundi huko aliko kuhakikisha ubora wa kazi yako
Sisi tunamlipa fundi kila anapomaliza steji fulani ya kazi na baada ya wewe kuafiki na umeridhika
Fundi anapokuja site ya mkoani basi utalazimika kumuandalia chumba cha kulala na tandiko la kawaida tu ila lenye utu
Fundi anapokuja site kwako, gharama za chakula ni juu yake fundi, wewe huhusiki kumuhudumia chakula
Fundi hausiki na kununua na kutunza vifaa site, kazi yake ni kujenga tuu kulingana na mchoro wa jengo husika
Wewe hauhusiki kukodi mashine za kazi kama mashine ya zege au shindilia
Boss unahusika kukodi/ kununua formwork na majukwa (scaffolding) ya kujengea
Ni haki na wajibu wa fundi kuweza kufanya kazi kwa weledi na kutunza nidhamu na heshima ya site kwako na anapolala
Kwa jambo au ishu yoyote ile kabla au pindi unapokuwa site tuwasiliane hapa mtandaoni
Ramani ni muunganiko wa michoro na vipimo vilivyoandaliwa na kuwekwa kitaalamu ili kuwasaidia wajenzi kujenga nyumba vile inavyotakiwa kulingana na msanifu alivyoandaa bila kukosea chochote. Pia ramani hutumika kufanya makadirio ujenzi, ni muongozo wa maongezi na majadiliano ktk ujenzi wako, huitajika serikalini kwajili ya taratibu nyingine na pia kupata kibali cha ujenzi, huhitajika pale unapoomba mkopo wa ujenzi benki...
Kurasa za ramani na kazi yake
Site plan -Â (ramani ya mpangilio wa kiwanja) hutumika ktk kuiweka nyumba sehemu sahihi ya kiwanja pale wanapoanza kujenga msingi. Pia huonesha vitu kama mashimo ya choo, geti, uelekeo wa nyumba, fensi.. zinapokaa
Floor plans - (ramani kuu ya nyumba) hizi ndizo hutumika kukata na kuonesha namna kuta, nguzo, madirisha, milango n.k vinavyokaa ktk nyumba
Rear elevations - (mchoro wa upande wa nyuma wa nyumba) hii huonesha namna nyumba upande wa nyuma inavyoonekana
Right side elevations -Â (mchoro wa upande wa kulia wa nyumba) hii huonesha namna nyumba upande wa kulia inavyoonekana
Left side elevations -Â (mchoro wa upande wa kushoto wa nyumba) hii huonesha namna nyumba upande wa kushoto inavyoonekana
Roof plans - (ramani ya paa) hizi hutumika kuonesha michoro na vipimo vya paa vinavyotakiwa viwe na kufuatwa wakati wa ujenzi.
Wastewater drawings - (michoro ya mashimo ya maji machafu) hii hutumika kuonesha namna na vipimo vya mashimo ya maji machafu yanavyotakiwa kujengwa; Mashimo kama soak-away pits, septic tanks, chambers...
Door and window schedules - (majedwari ya madirisha na milango) hii hutumika kuonesha vipimo na idadi ya madirisha na milango; Huweza kutumika kuanza kutengeneza madirisha na milango hata kabla ya ujenzi haujaanza maana vitu na ujenzi wote hufanyika ktk vipimo
Faida za Kujenga kwa Ramani Zetu
Ni mawazo ya wataalamu ujenzi ktk kujenga nyumba yako
Unajenga nyumba zinazoafiki mazingira na tamaduni zetu
Inatoa mwongozo wa kitaalamu wa kubadili idea kuwa uhalisia
Ni uhakikisho wa kuufuata ili kufanya shughuli ya ujenzi
Mwongozo wa marekebisho ktk ujenzi na ukarabati wako
Inatakiwa unapoomba kibali cha ujenzi serikalini
Inasaidia kuondoa mabishano na marumbano mnapojenga
Nyumba nzuri ya kisasa ambayo unaweza jenga popote panapofaa kwajili ya familia yako na mkafurahia wakati mzuri pamoja. Ina vyumba 3 jumla vya kulala ambapo viwili ni vyenye choo ndani; ina chumba kimoja cha kawaida. Ina choo na bafu za public, sebure, jiko, dining na veranda mbili.
There are no reviews yet.