MAANA YA SEBULE – INAPASWA IWEJE?

Sebule kwa kawaida ni sehemu ya ndani ya nyumba ambayo ni maalumu kwa kupumzikia, kujumuika na kupokelea wageni.  Kuna muingiliano wa maneno haya living room – sitting room – lounge – lounge room – front room kutegemea na eneo na mabadiliko ya kitamaduni. Maana ya sebule mimi binafsi nimeiona ipo katika KUPUMZIKA, KUJUMUIKA na KUPOKEA WAGENI.  Sebule sio chumba tu cha kawaida, ni sehemu yenye sifa zake muhimu! Je, sebule yako ina hizo sifa 3?

Sifa hizo tatu za sebule zimebebwa katika mambo mawili ya kitaalamu. Hivyo unapo andaa sebule yako kabla ya kuijenga ni lazima hivi vitu viwili viaangaliwe kwa umakini. Vitu hivyo ni

  • Mpangilio na Upande ilipowekwa kuhusiana na nyumba (orientation)
  • Mandhari/ Usanifu wa ndani wa hicho chumba (interior Design)

Mpangilio na Upande ilipowekwa kuhusiana na nyumba

  • Inakaribisha vipi wageni?
    • Je upande upi ukiiweka itakuwa inakaribisha wageni kwa uzuri Zaidi
    • Je mwonekano wake (sura) yake kwa nje ya jengo unakaribisha wageni?
  • Je, Sehemu ilipowekwa ina epusha kuona maeneo mengine ya nyumba ambayo hayapaswi kuonekana?
    • Maeneo kama chooni, bafuni, vyumbani n.k. kumbuka kuwa sebuleni ndipo wageni wanapofikia
  • Mpangilio na upande ilipowekwa kuhusiana na kupokea au kukinga Jua
    • Ni muhimu kujua unataka jua lipige sebuleni au laa! Je muda gani ungependa jua liipige sebule yako? Ni upande gani wa sebule ungependa uingize jua kwa muda fulani? Hivi ni vitu vya muhimu vya kufikiria ili upate ile ladha ambayo unaihitaji.
  • Kiasi cha mwanga na Mzunguko wa hewa
    • Kiasi gani cha mwanga ungependa kiingie ndani ya sebule yako? Upande upi wa sebule ungependa usipigwe na mwanga labda kwajili ya kuweka Luninga? Pia ungependa ka-upepo kaingie hadi sebuleni? Kiasi cha mzunguko wa hewa ungependa kiweje? Pia siku hizi watu wengi wanapendelea madirisha makubwa yaliyojaa kioo mpaka maeneo ya sakafuni; wengine wanapenda sebule yenye kubarizisha upepo!
  • Mtu akiwa ndani sebuleni, anaona nini nje?
    • Pia hilo ni jambo la msingi. Kulingana na mandhari ya kiwanja chako, ungependa mtu akiwa ndani sebuleni awe anaona nini nje? Je, ni bustani, maua, mawe au chemchem?
  • Utulivu na kelele
    • Mpangilio wa sebule unategemea pia kiasi cha utulivu ambao ungependa uwepo sebuleni. Pia ni muhimu kutazama kuwa sebuleni kunazalishwa kelele kiasi gani ambazo zinaweza kuathiri shughuli nyingine katika nyumba yako, mfano chumba cha kujisomea.

Mandhari/ Usanifu wa ndani wa hicho chumba

Rangi, mwanga, unyororo, mpangilio, mpishano, kimo, mfanano, ukubwa, umbile la Sebule na vitu vyake huathiri hali za watumiaji. Mpangilio wa vitu sebuleni huleta ladha fulani.

  • Ni vizuri sebule iwe na mwanga wa kutosha, hewa ya kutosha yenye kutia hamasa
  • Ni vyema sebule iwe inachangamsha, iwe inaleta hamasa ya kukaribisha wageni, hamasa ya maongezi, iwe inaleta uhali wa kupumzika. Isiwe inachosha, inaogopesha wala kuboa!

Mpangilio wa vitu na samani mbalimbali katika sebule unaleta ladha fulani! Maumbo ya hivyo vitu hubeba maana fulani na kuathiri hali za watumiaji. Ni muhimu kuchagua vitu vyenye kuleta ladha nzuri unayotaka katika sebule yako! Kutochagua hali unayoitaka katika sebule yako ni kumaanisha kuwa unaruhusu hali yeyote ile kuathiri watumiaji wa sebule yako, ambayo inaweza kuwa hali nzuri au mbaya! Amua sasa ni hali gani unataka iathiri watumiaji wa sebule yako!

  • Ungependa sebule yako iwe inaukubwa gani?
    • Ukubwa wa sebule unategemea pia kiasi cha watu ambao watakuwa wanatumia sebule, pia kiasi cha vitu ambavyo ungependa viwepo sebuleni. Umbali kati ya kochi na kochi, umbali kati ya kochi na luninga n.k huathiri ukubwa wa sebule yako. Ukubwa wa kiwanja chako pia unaathiri ukubwa wa sebule yako. Amua ukubwa wa nyumba yako kabla ya kununua kiwanja!

Mambo machache kuhusu rangi; rangi zinaweza sababisha hisia ya utofauti kwa binadamu na wanyama mbalimbali. Kwa hiyo unachagua rangi ya kutumia kulingana na aina gani ya uhali ambao unataka kuutengeneza katika chumba chako!

Unaweza kujiuliza, Kwanini alama za barabarani zina rangi ya njano/nyeupe kwa nyeusi? Rangi huathiri watoto, wazee, wageni n.k. Inaweza leta uchangamfu, uhuru, hofu n.k.

Msukumo hafifu wa rangi upo katika bluu, urujuani (rangi za ubaridi). Rangi zenye msukumo hafifu ni nzuri hata kupaka katika eneo kubwa. Ndio maaana rangi za njee za nyumba kama vile light blue hutumika kupaka nyumba. Fikili ingekuwa vipi nyumba ingepakwa rangi nyekundu tii!

Rangi zenye msukumo wa nguvu ni kama nyekundu, machungwa (orange), zambarau (purple) (rangi za ujoto). Pia rangi inaweza kuwa ina ugiza au mg’ao. Rangi zenye ubaridi na ugiza zikipakwa juu kama dari huweza leta hisia za kutisha (threatening).

Rangi nyeupe ni neutral, nyeupe huweza leta hisia za usafi, takasa, utaratibu. Rangi Nyeupe huendana na rangi mbalimbali.

Mtu fulani alijaribu kuonesha hali na athari mbalimbali zinazotokana na rangi; Usitumie hivihivi, zinahitaji utaalamu maalumu katika kutumia.

  • Nyekundu – Nguvu, shauku, kusisimua, changamfu
  • Machungwa (orange) – sisimua, shauku, tahadhari
  • Njano – changamsha, nguvu, Jua
  • Nyeupe – Usafi, takasa, utaratibu
  • Bluu – Asili , utulivu, shwari, raha, tiifu, maji
  • Waridi (pink) – furaha, utulivu
  • Kijani – asili, amani, mwafaka, upatanifu, shwari, afya
  • Zambarau (purple) – hadhi, mamlaka, ubunifu, mafanikio

Haya chini ni mapendekezo ya wataalamu fulani kuhusiana na rangi ambayo unaweza kupaka katika vyumba vya nyumba yako. Tumia wataalamu ili wakushauri namna ya kuzitumia ili utengeneze ladha nzuri

  • Sebuleni – rangi angavu za kuchangamsha zikichanganywa na vivuli pamoja na patterns. Rangi ya mchanga (beige), hudhurungi (tan) ukichanganya na Kijani au bluu. Hapo unahitaji mtaalamu ili akuchanganyie vizuri ili ilete ladha nzuri.
  • Chumba cha wazazi – ladha ya waridi (pink) ukichanganyia na kijani mpauko au bluu mpauko. Kuleta ladha ya upendo, ndoa na furaha!
  • Chumba cha wazee – rangi za uangavu kwani macho yao yamepungua nguvu ya kuona. Pia utumiaji wa ladha za kijani au bluu huleta hisia ya utulivu na uasili!
  • Chumba cha watoto – ladha ya rangi ya bluu, urujuani na kijani. Watoto wa kike wamekuwa wakipenda ladha ya rangi waridi. Kijani na bluu inafaa pia katika chumba cha kusomea!
  • Chumba cha maombi – Rangi zenye kuleta utulivu, rangi vivuli za bluu, urujuani, kijani
  • Chumba cha chakula – rangi zenye kuleta hamu ya kula kama rangi machungwa, nyekundu
  • Jikoni – rangi za usafi kama nyeupe
  • Bafuni – rangi za usafi kama nyeupe, grey ukichanganya na ladha ya kijani

Tumia samani, kuta, mimea maalumu, mapazia n.k katika kubeba rangi ambazo umekusudia.

Ni vyema kutengeneza sebule yako katika uzuri wake huku ukikumbuka kuwa sebule ni sehemu ya kupokelea wageni, kupumzikia na kujumuikia. Usisite kuwasiliana na wataalamu wako ili wapate kukusaidia kupata sebule yenye ubora wake.

mangula
Eng. Makazi Team
Makazi.ne.tz ni mtandao mahususi Afrika Mashariki wenye lengo ...
ID-15071
3
149 sqm
77 Pcs
14 m
2,667 Pcs
14 m
1,326 Pcs
ID-26509
3
70 sqm
51 Pcs
11 m
1,246 Pcs
8 m
619 Pcs
ID-10075
3
175 sqm
120 Pcs
12 m
3,366 Pcs
11 m
811 Pcs
ID-17529
3
195 sqm
134 Pcs
16 m
3,491 Pcs
15 m
1,736 Pcs
ID-17165
3
136 sqm
56 Pcs
15 m
3,259 Pcs
10 m
1,209 Pcs
ID-8174
4
135 sqm
95 Pcs
15 m
2,496 Pcs
12 m
1,273 Pcs
ID-8010
4
138 sqm
108 Pcs
15 m
2,160 Pcs
13 m
1,164 Pcs
ID-7823
3
84 sqm
65 Pcs
12 m
1,200 Pcs
9 m
645 Pcs
ID-20419
1
153 sqm
63 Pcs
15 m
3,672 Pcs
13 m
1,362 Pcs
ID-17121
3
177 sqm
122 Pcs
15 m
3,168 Pcs
14 m
1,575 Pcs
ID-15458
3
231 sqm
115 Pcs
17 m
5,068 Pcs
15 m
2,035 Pcs
ID-19158
1
212 sqm
87 Pcs
18 m
5,085 Pcs
14 m
1,886 Pcs
Makazi Icon Blue

Jiunge Uanachama

Jiunge uanachama ili uweze ona ramani ya mpangilio vyumba kabla hujanunua ramani kamili; Fahamu inahitaji PESA kiasi gani KUWEKEZA ktk biashara yako ili faida yake uitumie kama mtaji wa kujengea nyumba hiyo. Fahamu kiasi cha MKOPO UJENZI cha kuchukua na kurudisha kila mwezi ktk benki yako. Pia, utaweza ona GHARAMA za kujenga msingi, kuta, paa, dari, rangi, milango, madirisha... kwa nyumba zote ktk mtandao wetu, ili uweze CHAGUA, LINGANISHA, KUWEKA MIPANGO & MIKAKATI ya Jinsi ya Kuuendea Ujenzi Wako Vyema!