Kazi ya linta katika jengo

Linta ni moja ya kiungo katika jengo ambacho huwekwa juu ya sehemu zilizo achwa wazi katika kuta za jengo ili kubeba mzigo juu yake na kuupeleka salama mpaka katika maegemeo; ni kiungo kinachowekwa juu ya uwazi wa madirisha, milango, mageti n.k ili kuweza kubeba mzigo juu yake bila kunepa. Kiungo hiki ni muhimu kwani uwazi au kifaa kitakachojazwa katika uwazi huo kinakuwa hakina uwezo wa kutosha kubeba mzigo juu yake. Kazi ya linta ni sawa na kazi za mihimili (beam) na tao (arch) katika jengo, ijapokuwa linta hujengwa kiurahisi na kikawaida zaidi; haihitaji utaalamu sana. Linta hutumika pale ambapo mzigo unaobebwa sio mkubwa na pia urefu wa uwazi sio mkubwa; pale ambapo uwazi na mzigo ni mkubwa basi lazima utaalamu zaidi utumike na pia itumike mihimili au tao.

Kawaida Linta hubebwa juu ya tofali za jengo au mara nyingine juu ya nguzo za jengo; basi ni muhimu kuhakikisha kuwa ncha zake zinaingia na kufungwa vizuri katika kuta zinazobeba linta hiyo ili kuhakikisha linta ipo imara na kuta haziharibiki.

Kazi za linta

  1. Kubeba mzigo juu ya uwazi katika kuta

Hii ni kazi kubwa ambayo mara nyingi hutumika kufanya. Pale inapotokea juu ya dirisha au mlango unapaswa kujenga tofali nyingine au kuweka kitu chochote chenye uzito na fremu ya mlango haina uwezo wa kubeba mzigo huo, basi linta hutumika kubeba mzigo huo kwa ufanisi zaidi ili kuhakikisha uimara na ubora. Mara nyingi urefu wa linta katika majumba yetu huishia mita 3; pale umbali unapozidi 2m au mzigo kuwa mkubwa basi lazima hatua zaidi za kitaalamu zipate kufuatwa ili kuhakikisha hakuna kunepa wala nyufa katika linta yako.

Pale ambapo mzigo utakaobebwa ni mkubwa (tanki la maji, sakafu ya zege n.k) basi hatua za kitaalamu zinapaswa kuchukuliwa ili kuhakikisha kuwa uimara na usalama wa jengo lako.

  1. Kulishikilia na kulifunga jengo kiuimara

Linta pia hufanya kazi ya kulifunga jengo kwa pamoja ili liwe imara na lisitetereke kwa kuyumba, upepo, tetemeko n.k. Jengo linapokuwa limefungwa kwa pamoja na linta basi hufanya kazi kwa pamoja na kusaidia upande ule ambao ni dhaifu au umelemewa na mzigo uweze kustahimili. Bila linta, jengo linaweza kupunguza kutengemaa na uthabiti.

Kikawaida kuta za jengo zinapokuwa ndefu zaidi basi zinapunguza uimara wake; Lakini pale tunapozifunga kuta hizi kwa linta basi tunaziongezea uimara na uwezo wa kubeba mzigo.

Kwa nyumba zile za matofali ya kupachika (interlocking blocks), linta ni muhimu sana katika kuhakikisha tofali zinakaa kwa pamoja bila kupanguka. Linta pia inasaidia kuzishika kona za nyumba katika uimara.

  1. Kuzui nyufa katika jengo lako

Linta huzuia nyufa katika jengo lako zisivuke upande mwingine wa jengo. Linta hufanya kazi ya kuzikata nyufa hizo na kufanya upande mwingine wa jengo uwe salama. Uimara wa linta ndio unaofanya ufa usiendelee; pale ambapo nguvu ya ufa ikazidi uimara wa linta, basi upande mwingine nao utaupokea ule ufa. Ni muhimu kuhakikisha awali kuwa nyumba yako unaijenga vyema na kwa ubora ili nyufa zisitokee na kama zikitokea basi linta itakusaidia tuu kuzui nyufa zisiendelee. Pale inapotokea udongo katika kiwanja chako una hali ya ufinyanzi, basi ni muhimu kuiimarisha nyumba yako tangu katika msingi kwa kufunga nondo na maboresho mengine ili kuweza kuifanya nyumba yako kuweza kuhimili nguvu ya udongo mfinyanzi.

Aina za linta (materials)

Linta yaweza kutengenezwa kwa material mbalimbali kutegemeana na teknolojia, utaalamu, Upatikanaji wa malighafi n.k.

  1. Mawe bapa

Mawe yaliyobapa na katika umbo linalotakiwa huweza kutumika kufanya kazi ya linta katika jengo lako. Mawe yanaweza kuhitajika yachongwe vyema ili kuhakikisha umbo linalotakiwa linapatikana.

Utumiaji wa mawe ni mdogo sana na teknolojia hii imekuwa ikitumika miaka ya zamani zaidi haswa katika nchi za nje. Kikawaida ni vigumu kupata mawe yanayofaa kwa kazi hii hivyo huweza kuongeza gharama kwa kuongeza kuyachonga mawe yako.

Uimara wa mawe pia sio mkubwa kwa kazi kama hii hasa pale tunapotaka kufanyia kazi katika uwazi mrefu kwani mawe hayana uwezo wa kubeba umbali mrefu.

  1. Miti na mbao

Miti na mbao huweza kutumika kama linta katika jengo lako kama vitaweza kukidhi viwango vinavyotakiwa; baadhi ya viwango ni kutooza/kuharibika mapema, uwezo wa kubeba mzigo juu yake, kukidhi viwango vya moto n.k. Mbao na miti vimekuwa vikitumika maeneo mbalimbali tangu miaka ya zamani mpaka leo. Pale vinapotumika vizuri huweza kusaidia vyema kabisa katika jengo lako na kulifanya kuwa imara.

Kutokana na changamoto za gharama, uimara, kuoza, moto n.k matumizi yake yamepungua miaka ya sikuhizi katika majengo mbalimbali.

  1. Tofali

Pale tofali zinapopangwa vizuri na kitaalamu basi huweza kutumika kubeba mzigo juu ya uwazi salama kabisa. Utaalamu unahitajika katika upangaji wa tofali hizi. Mara nyingi aina ya tofali zinazotumika ni zile za kuchoma; ubora na uimara wake unahitajika ili kuhakikisha uimara wa linta itakayojengwa. Linta za tofali hazina uwezo mkubwa wa kubeba mzigo wa uwazi mrefu.

  1. Chuma

Bomba za chuma huweza kutumika kufanya kazi hii ya linta katika jengo lako katika ubora. Utaalamu unahitajika kuweza kupangilia vyema namna ya kutumika. Ni muhimu kuweza kuhakikisha usalama dhidi ya kutu na moto.

  1. Zege

Hii ni aina ya linta ambayo watu wengi wamekuwa wakitumia zaidi katika ujenzi wao. Linta hii mara nyingi huwekwa nondo ndani yake ili kuifanya imara na kuweza kubeba mzigo mkubwa na kwa umbali zaidi. Aina hii ya linta pia inasaidia kufanya nayo kazi kwa urahisi na kwa usalama zaidi dhidi ya moto, kutu na kuoza. Ni muhimu kuweza kuzipanga na kuzifunga nondo vizuri na pia kutumia zege iliyo katika kiwango kinachokubalika. Kwa nyumba zetu za kawaida, nondo za 12mm hulazwa mbili chini na mbili juu katika linta na kufungwa kwa ringi la 8mm na kufanya boksi la pembe nne kisha zege ya 1:2:4 humiminwa ili kutengeneza linta imara katika jengo lako. Linta ya zege inapofungwa katika kuta za jengo lako lote basi huweza kulifanya jengo lako litengemae kwa pamoja.

 

Mwisho, ni muhimu kuweza kujenga jengo lako katika ubora ili kuweza kuliongezea muda wa kudumu na kulifanya salama kwa kuishi. Ijapokuwa haya mambo yanahitaji utaalamu na yana gharama, ni muhimu kuweza kujenga na kuwekeza kwa faida. Linta katika jengo ni muhimu ili kuweza kulifanya jengo lako liwe imara na lenye kuvutia. Linta hulifanya jengo lako liwe imara na kulitengemaza kwa pamoja. Linta husaidia kuzuia nyufa kushambulia jengo lako. Ni muhimu kuweza kujenga jengo lako katika ubora kwajili ya usalama, uimara na uwekezaji.

mangula
Eng. Makazi Team
Makazi.ne.tz ni mtandao mahususi Afrika Mashariki wenye lengo ...
Tags: linta, lintel
ID-18256
4
273 sqm
0 Pcs
16 m
7,956 Pcs
14 m
2,990 Pcs
ID-15812
2
88 sqm
65 Pcs
12 m
1,575 Pcs
10 m
783 Pcs
ID-16831
3
261 sqm
180 Pcs
25 m
4,672 Pcs
13 m
2,323 Pcs
ID-17069
4
169 sqm
116 Pcs
15 m
3,025 Pcs
13 m
1,504 Pcs
ID-8010
4
138 sqm
108 Pcs
15 m
2,160 Pcs
13 m
1,164 Pcs
ID-19468
2
192 sqm
132 Pcs
16 m
3,437 Pcs
14 m
1,709 Pcs
ID-26211
4
186 sqm
154 Pcs
18 m
3,325 Pcs
13 m
1,653 Pcs
ID-17046
4
248 sqm
142 Pcs
21 m
3,862 Pcs
16 m
2,214 Pcs
ID-19172
3
118 sqm
48 Pcs
12 m
2,827 Pcs
10 m
1,048 Pcs
ID-17125
3
209 sqm
144 Pcs
17 m
3,741 Pcs
14 m
1,860 Pcs
ID-16443
3
190 sqm
131 Pcs
16 m
3,401 Pcs
15 m
1,691 Pcs
ID-26508
1
35 sqm
26 Pcs
7 m
700 Pcs
6 m
315 Pcs
Makazi Icon Blue

Jiunge Uanachama

Jiunge uanachama ili uweze ona ramani ya mpangilio vyumba kabla hujanunua ramani kamili; Fahamu inahitaji PESA kiasi gani KUWEKEZA ktk biashara yako ili faida yake uitumie kama mtaji wa kujengea nyumba hiyo. Fahamu kiasi cha MKOPO UJENZI cha kuchukua na kurudisha kila mwezi ktk benki yako. Pia, utaweza ona GHARAMA za kujenga msingi, kuta, paa, dari, rangi, milango, madirisha... kwa nyumba zote ktk mtandao wetu, ili uweze CHAGUA, LINGANISHA, KUWEKA MIPANGO & MIKAKATI ya Jinsi ya Kuuendea Ujenzi Wako Vyema!