Fahamu zaidi unapotaka kujenga nyumba bati zisizoonekana (Contemporary houses za Kitanzania)

CONTEMPOARY HOUSES nini?
– Contemporary maana yake ni MODERN. Hivyo hizi ni nyumba za kisasa zaidi (zinazo-trend)
– Zinasifa za kuwa simple, smart, minimalistic, clear. Zina sura bapa(planes), box style, nyuzi pembe nne, straightness, rangi chache zaidi nyeupe na gray, open space, less privacy as freedom, madirisha na milango mikubwa
– Zinatabia ya kutumia vifaa aina ya: zege, metal zaidi, vioo zaidi. Zimekuja katika zama hizi za matumizi makubwa ya viwanda na computer!
– Maghorofa mengi yanayojengwa siku hizi posta yana tabia hizi maana ni za kisasa
– Google picha: CONTEMPORARY HOUSES –> utapata jibu
– Watu wengi wanazipenda sana haswa. Nje ya nchi wanazijenga sana ila Tanzania watu bado hawana mwongozo zaidi

Tumekuandalia contempoary houses ambazo unaweza kujenga Tanzania huku tukiwa tumeangalia UCHUMI, TAMADUNI, HALI, UFUNDI… ambao upo katika mazingira yetu TANZANIA lakini pia bila kuharibu ladha, utamu, ubora… wa contemporary ili Mtanzania uweze uweze kupata maximum satsfaction na kutimiza hamu yako
– Tumeziweka zitumie bati la kawaida tuu ili kuepuka gharama za zege na nondo
– Bati limefichwa vizuri lisionekane ili lisiharibu ladha za muonekano
– Bati linakusanya maji na kumwaga ktk pembe zake nje bila kuvuja (kama nyumba za kawaida) [ila bati limefichwa vyema halionekani]
– Kutokana na kuziba bati lisionekane basi idadi ya tofali, cement imeongezeka kidogo. Hivyo gharama ipo kikawaida tuu
– Actually ni nyumba ya kawaida hivyo fundi wako anaweza kujenga vyema bila shida yoyote [cha msingi tu ajenge kulingana na ramani inavyosema]
– Watanzania tunajenga kwa awamu kidogo-kidogo, hata hizi waweza jenga kidogo-kidogo kwa awamu
– Mpangilio wa nyumba na layout ya vyumba umekaa katika tamaduni ya Kitanzania kwa welfare ya familia
– Ukubwa wa nyumba na vyumba ni wa kawaida katika kutosha katika viwanja vyetu

Kuziona zaidi nyumba hizi basi bofya hapa na uone nyumba kibao zenye makisio ya gharama na vifaa.

03/06/2019